Duration 9:27

MAGOLI YOTE: YANGA SC 3-2 KAGERA SUGAR (TPL – )

332 731 watched
0
858
Published 11 Apr 2019

Mabingwa wa kihistoria wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) Yanga SC wameendeleza rekodi yao ya ushindi kwenye uwanja wao wa nyumbani wa CCM Kirumba Jijini Mwanza baada ya leo kuwachapa Kagera Sugar mabao 3-2. Licha ya kutanguliwa, Yanga walitoka nyuma na kusawazisha kwa bao la kujifunga la Kassim Khamis dakika ya 35, kisha kufunga la pili dakika ya 48 kupitia kwa Heritier Makambo na la tatu likifungwa kwa ‘free-kick’ na Thaban Kamusoko dakika ya 72. Mabao ya Kagera Sugar yamefungwa na Paul Ngalyoma dakika ya 31 na Kassim Khamis dakika ya 58. Matokeo hayo yameifanya Yanga ifikishe pointi 74 kileleni mwa msimamo wa ligi huku Kagera Sugar wakisalia na pointi zao 36 katika nafasi ya 17. Haya hapa magoli yote kwenye mchezo huu.

Category

Show more

Comments - 132