Duration 8:27

Mhandisi Maryprisca Tatizo la Wasiofikiwa na Maji Dar es Salaam Kutatuliwa ndani ya Miaka Miwili

155 watched
0
1
Published 20 Jul 2021

#MbeyaYetuTv Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi amewahakikishia wananchi wanaopata huduma ya mjisafi na Salama kupitia Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es-salaam (DAWASA) ambao hawajafikiwa na huduma hiyo kuwa ndani ya miaka miwili maeneo yote yatapata huduma hiyo. Ameyasema hayo leo alipokuwa akikagua maboresho yaliyofanywa kwenye mitambo ya kuzalisha maji Ruvu Juu na Ruvu Chini Amesema maboresho hayo yamelenga kuhakikisha changamoto ya upatikanaji wa majisafi na salama katika maeneo yanayohudumiwa na DAWASA inaondoka kabisa. “ Maeneo yote mabayo hayajafikiwa na Maji tuendelee kuwa na subira. Tulikotoka ni mbali. Tunakokwenda ni karibu. Muda si mrefu maeneo yote yatapata maji bombani.” Amesema Mahundi. Amesema kwa sasa DAWASA wanatoa huduma ya Maji kwa asilimia 92 katika maeneo wanayoyahudumia, hadi kufikia mwaka 2023 maeneo yote yatakuwa yamefikiwa. Awali akitoa taarifa ya hali ya huduma ya Majisafi na salama Mkurugenzi Uzalishaji na Usambazaji Maji DAWASA Mhandisi Shaban Mkwanywe amesema mtambo wa Ruvu chini ulifanyiwa maboresho mwaka 2013 na kuwezesha ongezeko la upatikanajni wa Maji kutoka lita milioni 180 kwa siku hadi lita milioni 270 kwa siku wakati ule wa Ruvu Juu Matengezezo yalifanyika mwaka 2016 ambapo mtambo huo uliweza kuongeza upatikanaji wa Maji kutoka lita milioni 82 kwa sikuhadi lita milioni 196 kwa siku. “Sisi kama DAWASA tunaadhimia kuondoa kabisa tatizo la upatikanaji wa Maji katika jiji la Dar es salaam ifikapo mwaka 2023.” Amesema Mhandisi Mkwanywe. Kesho Naibu Waziri ataendelea na ziara ambapo atatembelea mradi wa Maji Chalinze-Mboga na mtambo wa kuzalisha Maji Wami

Category

Show more

Comments - 0