Duration 43:22

SHEIKH KILEMILE-MWISHO WA MAISHA YA VIUMBE

82 107 watched
0
441
Published 2 Sep 2015

Kitu chochote kilichoumbwa (kiumbe), bila shaka kina mwanzo na mwisho wake. Huo ni ukweli ambao kila mtu anaufahamu. Pia katika maandiko ya dini zote mwisho wa uhai huu tulionao kumeelezwa pia dalili na matukio yatakayosababisha uhai huu wa kila kitu kutoweka. Katika zama hizi za maendeleo ya sayansi na teknolojia, mwanadamu pia amejishughulisha na utafiti wa jinsi mwisho huu utakavyoweza kutokea. Ndiyo maana wasomi wa fani mbalimbali (wanasayansi na wabunifu wa michezo ya sinema) wakaja na dhana tofauti tofauti za jinsi mwisho wa uhai wa ulimwengu huu unavyoweza kutokea. Miongoni mwa dhana hizo zingine zilishatajwa na Mwenyezi Mungu ndani ya Qur’an yake. Katika documentary iliyoonyeshwa kwenye Television ya BBC hivi karibuni (April 2015), wanasayansi wametaja dalili ambazo zinaweza kusababisha kutoweka kwa uhai kuwa ni pamoja na; - uvamizi wa viumbe vipya kutoka angani (alien invasions), - mgongano wa sayari (asteroids), - jua kusambaratika na kupoteza nguvu zake, - kuibuka kwa volcano kubwa na matetemeko ya ardhi kila mahali, - kutokea kwa ajali za mitambo ya nuklia katika nchi zenye mitambo hiyo, - au programu za computer kwenda mrama hasa katika matumizi ya Robots, - kuibuka kwa magonjwa ya hatari (yatakayosababishwa na bakteria au virusi vipya kama tunavyoshuhudia vya ukimwi, ebola, n.k), - mabadiliko ya tabia nchi (na kusababisha mafuriko, ukame na njaa kali) na - mwishowe jambo ambalo wanalipa uwezekano zaidi ni kwa mwanadamu kujimaliza mwenyewe kwa matumizi ya silaha za maangamizi hasa za nuklia katika vita. Mwenyezi Mungu katika Kitabu chake Qur’an pia kathibitisha ukweli wa kutoweka kwa maisha haya pale aliposema kwamba kila kilichomo kwenye ardhi kitakwisha. Sasa fuatana na Sheikh Suleiman Kilemile kutoka Tanzania, anavyoielezea Mada hii kwa mujibu wa Uislam (kutoka ndani ya Qur’an na Sunna za Mtume Muhammad S.A.W) ili upate kuelimika……

Category

Show more

Comments - 78